Header

Q Boy ataitumiaje ‘Siku ya wapendanao’, Ametujibu hapa

Siku ya Kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa Mbunifu wa mitindo na Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya ‘Q Boy’ inaweza kutumika katika pande mbili katika maisha yake. Akiwa na mpenzi wake wanaweza kusherehekea ‘VALENTINES DAY’ lakini kama kimahusiano atakuwa Single kwa basi atasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Unataka kujua Mahusiano ya Q Boy yakoje? Tulia!, Akizungumza na Dizzim Online, Q Boy amesema kuwa, siku ya leo kwake ataitumia kwa kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kwakuwa Valentines imewadia akiwa Single.

“Siku ya kuzaliwa kwanza naithamini sana kwasababu ni kati ya sherehe kubwa za kuanza kwa maisha yangu, niko Single na of course nitaienzi siku ya kuzaliwa kwangu. Uzuri furaha inabaki pale pale, kwanza ni mwenye Afya njema hivyo I cant complain” Amesema Q Boy.

Hata hivyo Q Boy amegusia pia juu utaratibu wake wa kuachia kazi mpya baada ya kuachia ‘Kamoyo’ iliyomshirikisha Mr. Blue na kuongeza kuwa amaanini kinachofanyika kwa sasa katika muziki wa Tanzania ni kitu kizuri na katika kuusoma mchezo anaona bado anahitaji kuwapa muda wenye utayari wa kuachia kazi zao ili akiamua kutoa iwe ni kazi ya tofauti na za wasanii wenzake.

“Mipango yangu kwa mwaka 2018 ni kuachia kazi nzuri zaidi ya nilizokwisha achia, na kwa sasa hivi navuta upepo ili kuhakikisha sitoi kazi ya kufanana na kazi ya wasanii wenzangu kuaniza wazo la wimbo mpaka miondoko. Nimejipanga kuwa tofauti sana na nalisoma Game kwa umakini mpaka nikijiridhisha na kuona sasa ni muda wangu” Alimalizia

Comments

comments

You may also like ...