Header

Bahati baada ya kupata mtoto wa kike, kuwapa mashabiki zawadi

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Kevin Kioko ‘Bahati’ ametangaza ujio wa wimbo wake mpya baada ya kupata mtoto wake wa kwanza wa kike kwa jina ‘Heaven Bahati’ siku ya wapendanao(Valentine’s Day) na mpenzi wake Diana Marua.

Akitangaza ujio wa kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ten Over Ten’, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati aliweka kava ya wimbo huo ambayo anaonekana yeye na mpenzi wake na kuwataka mashabiki wakae tayari kupokea kazi mpya kutoka kwake.

Kilichoongeza shahuku ya mashabiki kusubiria kwa hamu ujio wa wimbo wake huo ni picha iliyotumika kupamba kava ya wimbo huo kwakuwa kila mmoja ashaanza kutabiri kuwa inawezekana Diana katumika katika video kama video queen kipindi ambacho alikuwa ni mjamzito.

Bahati anayetarajia kutambulisha rasmi makao makuu mapya ya lebo ya Studio yake ya EMB Recrds ambayo katika ukubwa inatazamwa kuja kuwa moya studio kuwa katika ukanda wa Studio zinazopatikana Afrika Mashariki.

 

Comments

comments

You may also like ...