Header

Davido aendeleza kasi yake Mtandaoni kwa kazi yake mpya

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’ ameanza vyema ukurasa wa kuachia ngoma kwa kasi ya utazamwaji wa video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Flora My Flawa’ iliyoongozwa na Director ‘CLARENCE PETERS’.

Hatua hii imekuwa ni habari njema kwa Davido na mashabiki wa muziki wake ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter aliweka tweet ya kuonesha kuwa video ya wimbo wake huo imefikia kutazamwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya masaa 48.

Davido kwa mwaka jana aliweza kufikisha watazamaji Milioni 100+ katika mtandao wa YouTube kupitia video rasmi za nyimbo alizoachia kwa mwaka mzima na kwa mwanzo huu wa kazi yake ya ‘Flora My Flawa’ inategemewa kuwa Davido ataingia katika rekodi nyingine nzuri kama mwendo wa kuachia nyimbo utakuwa kama ilivyokuwa mwaka jana.

Comments

comments

You may also like ...