Header

Tangazo la Ndoa ya Diamond Platnumz kutoka kwa Babu Tale laingiliwa na Zari

Siku ya wapendanao(Valentine’s Day) imekuwa ya uzuni kwa Zari The BossLady na hilo lilibainia mara tu baada ya kuweka ujumbe mtandaoni kuwa ameachana rasmi na Diamond Planumz na anabaki kuwa naye kama baba wa watoto wake wawili na mzazi mwezake tu na sio wapenzi tena.

Zari katika kubayanisha kilichochangia kwake kuchukua maamuzi hayo ni pamoja na kukithiri kwa vumi na ushahidi wa vitendo vya usaliti uliokuwa ukitekelezwa na Diamond Platnumz na ujumbe wa maamuzi hayo magumu na ya kutia uchungu lakini ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa amembidi kufanya hivyo ili aweze kulinda heshima yake na utu wake.

Understand that this is very difficult for me to do. There have been multiple rumors some with evidence floating around in ALL SORTS of media in regards to Diamond’s constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised. We are separating as partners but not as parents. This doesn’t reduce me as a self-made individual, and as a caring mother, and the boss lady you have all come to know. I will continue to build as a mogul, i will inspire the world of women to become boss ladies too. I will teach my four sons to always respect women, and teach my daughter what self-respect means. Unlike many, I’ve been in the entertainment industry for 12 years, and through all my challenges I came out a victor because I am a winner, and so are all of you Zari supporters. HAPPY VALENTINE'S

A post shared by Zari (@zarithebosslady) on

Kwa lugha ya kueleweka kwa wanaAfrika Mashariki, Aliandika “Ni jambo lenye ugumu kwa mimi kufan  ya.Kumekuwa na uvumi mwingi na ushahidi uliozunguka katika vyombo vya habari kuhusiana na usaliti wa mara kwa mara wa Diamond. Kwa masikitiko nimeamua kuvunja uhusiano wangu na Diamond, Heshima utu pamoja na Ustawi wangu haviwezi kuchezewa na kuharibiwa.

Tunawatengana kama wapenzi lakini sio kama wazazi.

Hii hainipunguzii kitu kama mtu niliyejjitengeneza mwenye, kama mama mwenye kujali, na mwanamke mwenye kujiweza ambaye umemjua.

Nitaendelea kujenga kama mfanya biashara na mtu aliyefanikiwa, nitahamasisha ulimwengu wa wanawake kuwa wanawake wenye kujiweza pia.

Nitawafundisha watoto  wangu wanne kuwaheshimu wanawake daima, na kufundisha binti yangu njia gani ya kujiheshimu.

Tofauti na wengine wengi, nimekuwa katika sekta ya burudani kwa miaka 12 sasa, na nimekuwa ni mwenye kupitia changamoto nyingi na kuibuka kwakuwa mimi ni mshindi, na ninyi pia ambao ni wafuasi wa Zari.

HAPPY VALENTINE’S”.

Basi hili lilimaanisha moja kwa moja kuwa kauli ya tangazo lililotolewa na meneja wa Diamond Platnumz ‘Babu Tale’ siku ya kufunga ndoa ya Dj wa Diamond Platnumz ‘Romy Jones’, kuwa Diamond platnumz na Zari watafunga ndoa zimeyumbishwa na tangazo la Zari la kuachana rasmi na Daimond.

Siku ya sherehe ya kufunga ndoa ya Romy na mkewe iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana, Babu Tale alitangaza kuwa siku sio nyingi Diamond Platnumz na Zari the BossLady watafunga ndoa. Itazame video ya tamko la Babu Tale.

Comments

comments

You may also like ...