Header

Otile Brown atamani kinachofanyika Tanzania, Kifanyike Kenya pia

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, Otile Brown ametaja utofauti iliyopo ya kimuziki kati ya mapokeo ya kazi za muziki kwa mashabiki nchini Tanzania na nchini Kenya hasa pale msanii anapoachia kazi zaidi ya moja ndani ya muda mfupi.

Instagram/OTILE BRWON Otile Brown akiwa Jukwaani

Akipiga Stori na Redio Maisha ya nchini humo, Otile amesema kuwa muziki wa Tanzania una nguvu kubwa na mashabiki wanaweza kupokea kazi za wasanii bila kuchoka kwakuwa wasanii wanazingatia ubora wa kazi ambazo haziwachoshi mashabiki kusikiliza.

Vile vile Otile ameweka msisitizo kwa wasanii kufanya kazi zitakazo ishi muda mrefu na mashabiki kuwa na moyo wa kumpa support msanii wanayempenda kwani anaamini kama itafanyika hivyo, itachangia kwa kiasi kikubwa muziki wa Kenya kukua na kuingia katika ushindani mzuri wa kibiashara na mataifa makubwa ambayo yameshakua kimuziki.

Hata hivyo Otile aliongeza kuwa, moja ya chachu zitakazoongeza thamani ya muziki wa Kenya ni ushirikiano wa Tanzania na nchi ya Kenya katika bishara ya muziki ambapo amegusia ujio na mipango iliyopo ya ufunguaji wa tawi la lebo ya muziki ya WCB WASAFI, taarifa zilizotolewa na mmiliki wa lebo hiyo ‘Diamond Platnumz’ wiki hii.

Comments

comments

You may also like ...