Header

Idris Sultan aitamani nafasi ya maisha ya Jela ya Papii Kocha

Muigizaji, mchekeshaji na Mtangazaji wa redio na Tv kutoka Tanzania, Idris Sultan amerusha karata yake ya Bahati ili apewa nafasi ya kucheza nafasi ya maisha ya jela ya Mwimbaji wa muziki wa dansi, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Staa huyo wa filamu ameiambia kampuni inayofanya kazi na Papii ‘Wanene Entertainment’ kuandaa muongozo(Script) wa maisha ya Papii Kocha naye yuko tayari kama muigizaji kushiriki.

“Wanene andikeni script ya movie ya maisha ya Papii Kocha, I am ready” alindika Idris Sultan.

Kilichoweka msisitiza wa kuwa Idris anaitamani nafasi ya Papii Kocha hasa nafasi ya maisha ya Jela ni vazi alilovaa katika picha aliyopost kufanana na moja ya vazi la Papii katika Video ya wimbo wake ‘Waambie’ vazi lililobeba maudhui ya maisha ya jela.

Wazo hili la Idris limeibuka katika ujio wa ngoma mpya ya Papii Kocha ‘Waambie’ inayotoa ushuhuda wa walichokipa tafsiri ya maajabu juu yake na Baba kuachiwa uhuru kutoka katika adhabu ya kifungo cha maisha Jela baada ya kutumikia takribani miaka 14.

Wanene Entertainment inamilika studio ya kisasa ya muziki na vifaa za kiasasa vya uandaaji wa kazi za sanaa zenye ubunifu kwa njia ya utunzaji wa kumbukumbu katika mfumo wa picha.

 

Comments

comments

You may also like ...