Header

Nay wa Mitego awateka kwa Silaha ili waweke Mikono Juu

Anatambulika kama Msanii wa muziki wa rap kutoka Tanzania na mwenyewe kujiita half-caste wa kinyakyusa na ki-chagga, kwasasa atajisikia poa kama ukimuita ‘Baba Yaga’. Kutoka kwake kuja kwako ni kazi yake mpya kwa jina ‘Mikono Juu’ chini ya utayarishaji wa Prodyuza Awesome kutoka Studio za Free Nation(Free Nation Records).

Mbali na kuwa Nay katika wimbo huo anasikika Akisema “Hatuli mtaji sisi tunatumia faida” lakini kwa vizuri vyote vilivyoonekana katika video yake ni wazi ametumia Mtaji wa kueleweka ambapo Video ya wimbo huo imeongozwa pia kukamilishwa na Director Nicklass.

Wazo la wimbo huo chini ya Nicklass imeonekana walioshiriki walifanya kila walichokifanya ikiwa ni pamoja na uwekaji mikono juu na kukata viuno kwa shinikizo la silaha za moto(Mfano) walizobeba warembo waliopewa jukumu la utekaji sambamba na Nay kuonekana kubeba Bastora(Mfano).

Comments

comments

You may also like ...