Header

Rayvanny awatambulisha Rasmi Jason Derulo na French Montana kwenye muziki wa Bongo Fleva

‘Tip Toe’ kutoka kwa Staa wa muziki nchini Marekani, Jason Joel Desrouleaux ‘Jason Derulo’ imekuwa ni ngoma ambayo ndani ya miezi miwili imepata watazamaji zaidi ya Milioni 66+ kwenye mtandao wa YouTube na baada ya kumshirikisha French Montana, sasa imetoka rasmi Remix yake ikiwa imemshirikisha Staa wa ngoma ya Kwetu kutoka Tanzania ‘Rayvanny’.

Rayvanny anakuwa msanii aliyeingia kwenye masikio ya wengi mwaka 2016 chini ya lebo ya WCB Wasafi anayepata kolabo na mastaa wakubwa Afrika na Dunia na moja ya kikubwa mwaka 2017 alifanikiwa kuleta tuzo ya BET nchini Tanzania kwa mara ya kwanza kupitia kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act Artist’. Moja ya mahojiano na Dizzim Online, Rayvanny aligusia uwezekanao wake wa kuingia Studio kikazi na wanakikundi cha muziki nchini Marekani ‘Migos’.

Msikilize RayVanny alipogusia uwezekano wake wa kufanya kazi na wanakundi la Migos.

Hata hivyo huu ni mwanzo mzuri kwa Rayvanny kuelekea kulitangaza taifa la Tanzania katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na Tip Toe Remix inaweza kumtengenezea hali ya kuaminika kwa French Montana na mastaa wengine wa Mataifa ya mbali na Tanzania.

Tip Toe Remix.

Comments

comments

You may also like ...