Header

Wema atoa ya moyoni kwa Diamond na Zari

Msanii kutoka Bongo Movie nchini Wema Abraham Sepetu ametoa ushauri juu ya mahusiano ya aliyewai kuwa Mpenzi wake ambaye ni Staa wa Muziki Diamond Platnumz na mzazi mwenzie Zarina Hasani a.k.a ZaritheBosslady baada ya Zari kukiri kutokuwa tena kwenye mahusiano ya kimapenzi Diamond.

Akipiga story na Dizzim Online Mrembo huyo amesema bora wamalize tofauti zao ili waendelee kuwalea watoto wao kwa pamoja kwasababu hakuna mahusiano yasiyokuwa na changamoto wala migogoro.

“Kama kweli wameachana mimi naona wayamalize tu na maisha yaendelee ingawa mapenzi hayaingiliwi  warudiane ili walee watoto wao kwa pamoja” Amesisitiza mrembo huyo mwenye mashabiki wengi nchini Tanzania.

Pia Mrembo huyo amegusia suala la kupotelewa na Akaunti yake ya Instagram na kusema kuwa ni kweli imechukuliwa na amewaomba Mashabiki zake waendelee kuwa na moyo wa subira kwani bado anaendelea na jitihada za kuirudisha mikononi mwake.

Comments

comments

You may also like ...