Header

Emmanuella Samuel adaka shavu la Hollywood akiwa na miaka 7

Mtoto Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Nigeria, Emmanuella Samuel, amepata dili la kufanya kazi na kampuni kubwa ya kuandaa filamu za watoto, Disney nchini Marekani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Emanuella mwenye umri wa miaka saba ameweka picha iliyomuonesha akiwa katika mazingira ya kuandaa wa filamu  na kuandika “Thanks @disneystudios God bless everyone whose support has added to bringing us here. I never dreamed of being here so soon. I miss Success. I love you all.”.

Hata hivyo Emmanuella amepata pongezi kutoka watu maarufu na pongezi ilionekana mtoto amepiga hatua kubwa katikaumri mdogo ni kutoka kwa  rais wa bunge la senate wa Nigeria.

Vile vile  Emmanuella ni mchekeshaji mwenye umri mdogo na kwanza kutoka Afrika kuwa na wafuasi milioni moja kwenye channel yake ya video na kazi zake za uchekeshaji kwenye mtandao wa Youtube.

Comments

comments

You may also like ...