Header

Mbosso aliwezaje kuwakalisha mafala??!!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Mbwana Yusuph Kilungi ‘Mbosso’, tarehe 28 Januari mwaka huu alitambulishwa rasmi kama msanii atakayekuwa chini ya utendaji kazi za muziki wa lebo ya WCB Wasafi na utambulisho wake uliambatana na kazi yake inayokwenda kwa jina ‘Watakubali’.

Katika uandishi wa wimbo huo wa kwanza kutoka kwake kama msanii wa kujitegemea(Solo Artist), kwa mujibu wa wazo la wimbo Mbosso anasikika katika bridge baada ubeti wa kwanza akiuliza utambulisho wake kwa wazazi wa mpenzi wake atachukuliwaje ikizingatiwa kuwa alishawafanyia matukio ya wizi pia kielimu yeye ni mjinga?

“Na vipi kuhusu wazazi wako, Kielimu mimi mjinga/ Japo mapenzi haya Hayanaga kasoro” kisha kupitia neno lile lile la UJINGA, Mbosso katika kiitikio akisema “Nawakalisha mafala, ‘Wajinga’ wakuja Bongo…Wageni wa Dar es Salaam”.

Hapa ndo Swali likaibuka kuwa kwa sanaa yake ya uandishi alimaanisha nini kwa matumizi ya neno ‘UJINGA’ ikiwa maana halisi ya neno hilo ni ‘Mtu asiyejua kitu au jambo Fulani au neno lenye maana ya dharau au tusi kwa anayechukuliwa kutojua kitu’ na kama yeye alikuwa Mjinga aliweza kukalisha mafala???!.

Isikilize utupe kile ulichokielewa kwa maana ya Mbosso kuwa mjinga na akaweza kuwakalisha mafala.

Comments

comments

You may also like ...