Header

MSANII BEKA THE BOY KUTOKA KENYA ANAKUALIKA KUSIKILIZA KIBAO KIPYA- NIME FALL!

 

Msanii Beka The Boy anazidi kuwasha moto kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Kenya huku akiwa anaiwakilisha vyema Pwani ya Kenya kama msanii pekee mwenye juhudi za kupamabana na ushindani uliopoa kwenye game ya muziki Arica Mashariki. Kwasasa Beka The Boy ndiye msanii anayetegemewa na mashabiki wa Pwani ya Kenya haswa baada ya msanii Otile Brown kujitoa kwenye kundi la wasanii wanao iwakilisha Pwani ya Kenya na kuamua kuwakilisha Mkoa wa Nyanza ambako huko ndiko anasema ni chimbuko lake. Beka kwasasa ameachia kibao kipya kwa jina”Nime-fall” na hii nibaada ya hivi majuzi kuachia kibao chengine ambacho hadi sasa bado kinafanya vyema kwenye mesia za nchini Kenya, akiwa ameshirikiana na msanii mwenza kutoka Pwani ya Kenya vivyo hivyo kwa jina Kigoto Mbonde.

Beka ambaye kwa kasi yake ya kutoa muziki kila mara, anakisiwa kuwatia tumbo joto wasanii magwiji walio bobea kwa mda kwenye ramani ya muziki wa Pwani ya Kenya wakiwemo wakina Susumila, Chikuzee, Sudi Boy na wengine wengi. Muziki wa Pwani ya Kenya umekuwa na ukaribu sana na ule wa Bongo Fla kwani Kiswahili kimekuwa kikitumika kwa kina katika kutunga mashairi kwenye nyimbo kinyume na muziki unaotoka bara ya Kenya, nikimaanisha jiji la Nairobi na miji mingine inayopatikana katika nyanda za juu za nchi ya Kenya. Hivyo kuifanya sanaa ya muziki wa Bongo kutamba na kusambaa kwa haraka katika miji ya Pwani ya Kenya na viunga vyake na pia kuwavutia wasanii wa Pwani ya Kenya kama Beka The Boy na wengine wengi kufata muundo msingi wa wasanii wa Bongo wanavyofanya kama vile mtindo wa kuachia vibao vikali kwa mkuropuko ili kuwapa mashabiki wake nafasi ya kufurahia utamu wa muziki kila uchao. Hebu mpe sikio lako aweze kukuburudisha na kibao hiki kipya nimekusogezea hapa chini.

Comments

comments

You may also like ...