Header

Kagwe Mungai apaa mpaka Nigeria, Akutana na ‘Niniola’

Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Kagwe Mungai amemshirikisha Staa wa uimbaji kutoka nchini Nigeria ‘Niniola’ kwenye ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Till the End’ chini ya ‘Taurus Musik’.

Taurus Musik ni lebo inayomsimamia Kagwe na katika usimamizi imetimiza jukumu lake ambapo wimbo huu umetayarishwa na Atwal Music ya nchini Kenya huku video ikiongozwa na Director ‘Stanz’ Stanz Visuals kutoka nchini humo.

Kagwe anafanya kazi chini Taurus Musik na mastaa wengine kutoka Afrika Mashairiki ambao ni pamoja na Lady JayDee kutoka Tanzania, Alicios Theluji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kutoka katika lebo hiyo ameshashirikiana na Mwimbaji Alicious katika wimbo unaokwenda kwa jina ‘Nyumbani’ uliotoka mwaka jana.

Comments

comments

You may also like ...