Header

Lupita Nyong’o kucheza nafasi ya Mama Trevor Noah kwenye ‘Born a Crime’

Staa maigizo na mshindi wa tuzo ya Oscar  mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyong’o anatarajia kushiriki katika filamu ya kitabu cha ‘Born a Crime’ kinacho simulia maisha ya mchekeshaji maarufu, raia wa Afrika Kusini, Trevor Noah.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lupita aliweka picha yake akiwa na Trevor Noah kisha katika maelezo sambamba na picha hiyo alithibitisha kuwa ataichukua nafasi ya kuigiza kama mama mzazi wa Trevor katika filamu ya maisha ya Mchekeshaji huyo.

“Nilipokisoma kitabu Sikuweza kukiweka chini. Ninafuraha kutangaza kuwa nitahusika kama mkuu na kutayarisha filamu juu ya kitabu hicho!” Lupita Nyong’o aliandika katika Ukurasa wake wa Instagram.

Kitabu hicho cha ‘Born a Crime’ kumebeba simulizi ya maisha ya Trevor Noah aliyekulia katika enzi za ubaguzi nchini Afrika Kusini kama mtoto aliyezaliwa na mwanamke mweusi kwa baba mzungu.

Comments

comments

You may also like ...