Header

Majibu ya Bill Nass kuhusu kazi zake na Uongozi wake

Msanii wa Muziki wa Hip Hop nchini Tanzania Bill Nass, ameizungumzia mikakati yake juu ya muziki wake kwa sasa.

Akipiga story na Dizzim Online Rapper huyo ambae tayari ameshaachia ngoma yake inayoitwa ‘Tagi Ubavu’ amesema kwasasa kasi aliyoanza nayo ndio hiyo hiyo kikubwa ni Mashabiki kuzidi kumpa ushirikiano.

“Ndio tumeanza hivi na natumaini tutanedelea hivi hivi kikubwa ni sapport ya Media pamoja na mashabiki tunaweza kuendelea na kufanya vikubwa tena zaidi ya hivi naamini nafanya muziki mzuri na wenye mashabiki” Amesema msanii huyo.

Aidha Bill Nass ameshindwa kuzungumzia mahusiano yake na Meneja wake Petitman na kueleza kuwa mashabiki waangalie kazi zake tu kwasasa.

 

Comments

comments

You may also like ...