Header

Ricardo Momo amrusha Diamond Platnumz kwa wanawake

 

Meneja wa msanii Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ na msimamizi wa baadhi ya majukumu ya wasanii kutoka lebo ya WCB Wasafi, Ricardo Momo amemtumia Diamond Platnumz kama mfano wa kile kinachozingatiwa na wanachopenda wanawake katika maisha yao ya uhitaji.

Akitumia picha ya miaka ya nyuma ya Staa huyo wa muzki Bongo Fleva(#TBT), Meneja huyo ameandika kuwa kila mwanaume sio chaguo la Mwanamke bali mwanamke anapenda kuweka ukaribu na  mwanaume mwenye mvuto na anayeelea katika bahari ya maendeleo na mafanikio.

“”Wanawake Hawapendi Kila Mwanaume Bali Wanapenda Mwanaume Mwenye Maendeleo Na Mvuto Kwenye Jamiii..!! Aliandika Richard Momo.

Hata hivyo Diamond Platnumz ni msanii kutoka Tanzania ambaye kwa sasa anatambulika kimataifa katika baadhi ya mataifa kwa sasa, anazungumzwa na kupendwa zaidi na wanawake tofauti na kipindi cha nyuma jambo ambalo linaweza kuwa ni chanzo na mchango wa mawazo ya Ricardo ya ujumbe alioundika.

Vil;e vile mbali na Diamond Platnumz kuwa karibu na meneja Momo, siku mbili zilizopita ilikuwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake na mpaka sasa mashabiki hajawakutana ujumbe wa Diamond Platnumz akimtakia heri ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake mpaka sasa hasa mtandaoni ambako waliowengi ushuhudia akifanya hivyo kwa watu wake wa karibu.

Comments

comments

You may also like ...