Header

Beki wa zamani wa Arsenal na Man City amtabiria Ubingwa Guardiola mbele ya Wenger

Beki wa zamani wa Vilabu vya Arsenal pamoja na Manchester City Kolo Toure ameweka wazi utabiri wake juu ya Fainali ya Kombe la EFL kati ya Man City dhidi ya Arsenal itakayopigwa Siku ya Jumapili katika Dimba la Wembley.

Toure, 36 ambaye amewai Vitumikia Vilabu hivyo viwili kwa wakati tofauti(Arsenal 2002-2009 Man City 2009-2013) amesema kwa upande wake anawapa nafasi Klabu ya Man City kutwaa Ubingwa huo kutokana na kiwango walichonacho Msimu huu kwenye Ligi lakini pia katika Mashindano ya Ulaya.

“Timu zote zinacheza Mpira mzuri, Toure alikiambia kituo cha Sky Sports News. Arsenal ina Wachezaji wengi wenye uzoefu wa kucheza Fainali, hili ni Jambo Moja lakini ukiniuliza mimi ni timu gani nahisi itashinda Mchezo huo, nitaipa Man City. City kwa sasa Wanacheza Mpira mzuri sana katika Ligi lakini pia katika Mashindano ya Ulaya, wanacheza vizuri sana, kama Watacheza kama walivyocheza kwenye Michezo ya nyuma kwa kiwango kile, hakutakuwa na kitu chochote cha kuwazuia kwa kweli”. Alisema Toure

Man City chini ya Pep Guadiola itashuka katika Uwanja wa Wembley kwenye Mchezo huo wa fainali ikitafuta ubingwa wake wa kwanza tangu Guadiola ajiunge na kikosi hicho huku Arsene Wenger akitafuta Kombe lake la kwanza la EFL tangu aanze kuifundisha Arsenal(hajawai shinda Ubingwa wa EFL).

Comments

comments

You may also like ...