Header

Michy Batshuayi akiri kufanyiwa ubaguzi wa rangi na Mashabiki nchini Italia

Mshambuliaji wa chelsea ambaye yupo kwa Mkopo katika Klabu ya Borussia Dortmund Michy Batshuayi amethibitisha kufanyiwa ubaguzi wa rangi kutoka kwa Mashabiki wa Klabu ya Atlanta wakati wa Mchezo wa Kombe la Europa dhidi ya Atlanta siku ya Jana.

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa kijamii wa Twitter Staa huyo kutoka Ubelgiji aliweka ujumbe punde tu baada ya Mchezo kumalizika ambao Dortmund ilitoka sare ya 1-1 na kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 kwa Faida ya ushindi wa 3-2 kwenye uwanja wao wa Nyumbani.

Batshuayi ameweka ujumbe huo wenye maana ya kushangazwa na Mashabiki wa Klabu hiyo kupiga kelele za Nyani kwake wakiashiria ubaguzi wa rangi huku akiwaachia kauli ya kebehi kuwa Dortmund imefuzu hatua inayofuata ya Europa lakini Mashabiki wa Atlanta wataisha kuangalia Michuano hiyo kwenye TV tu kwani tayari wametolewa kwenye Mashindano hayo lakini pia amewakumbushia Mashabiki hao kutazama Movi mpya ya BlackPanther.

Kumekuwa na Mfululizo wa matukio ya Ubaguzi wa rangi nchini Italia hususani katika Ligi kuu nchini Italia ambayo wamekuwa wakifanyiwa Wachezaji wengi wa Afrika wanaocheza Ligi hiyo akiwemo Balloteli.

Comments

comments

You may also like ...