Header

MwanaFA ataja cha kufanya kama angekuwa waziri katika wizara ya sanaa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ ameweka wazi ya anachoweza kukifanyia mamabdiliko katika sekta ya sanaa kama angekuwa Waziri wa Sanaa Tanzania.

FA alionesha kutamani kufanya mabadiliko kwa kuhakikisha wasanii wa muziki wanafaidika kupitia kazi zao za sana kwa kulipwa mirabaha kutoka kwenye vituo mbalimbali vya matangazo(Televisheni na Redio) pamoja na sehemu za Umma zinazotumia kazi za wasanii kibiashara.

Hata hivyo mfumo huo aliougusia Mwana FA, unafanya kazi nchini Kenya kwa wasanii wanaofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya matangazo ambapo wapo wasanii baadhi kutoka Tanzania wanalipwa kiasi iikubwa kupitia nyimbo zao kuchezwa nchini humo.’

 

 

 

Chanzo: Clouds Media

Comments

comments

You may also like ...