Header

Tiwa Savage alipa deni la kazi aliyoahidi akiwa na Omarion

Mrembo na Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria chini ya lebo ya Mavin Records, Tiwatope Savage-Balogun ‘Tiwa Savage’ ameachia kazi yake mpya kwa jina ‘Get It Now’ iliyosubiriwa kutoka kwenye album yake ya ‘Sugarcane’ iliyotoka rasmi mwaka jana.

Itakumbukwa kuwa Januari 25 mwaka huu Tiwa aliweka picha mtandaoni kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na Staa wa muziki kutoka Marekani, Omarion na kuuliza ni wimbo upi wa ufuate kutoka kwenye album hiyo, swali ambalo limejibiwa kwa kazi hiyo mpya iliyotoka sambamba na video.

Tiwa katika Post ya swali la kuwa ni video ya ngoma ipi ifuate aliweka kiashiria cha kuwa wawili hao kuna uwezekano wa kushirikiana ‘Tiwa Savage x Omarion’.

Comments

comments

You may also like ...