Header

Vibe Records yahusika kumuombea Radhi Aslay

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Aslay Isihaka Nassoro ‘Aslay’ ameachia kazi yake mpya kwa jina ‘Nibebe’ chini ya utayarishaji wa Prodyuza Shirko kutoka Studio ya Vibe Records ambapo ujio huo umetoka kwa lengo la kuwataka radhi mashabiki juu ucheleweshaji wa kazi kutoka kwa Aslay.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa studio hiyo, yameandikwa maneno kuwa kazi hiyo mpya inatoka na inawataka radhi mashabiki kwa ukimya wa Aslay kuchelewa kuachia wimbo wake pekee yake bila kumshirikisha msanii.

“@aslayisihaka ashafanya yake tayari kuachia wimbo wake #Nibebe hii ni kwaajili ya kuwataka radhi mashabiki kwa kimya ambacho hawajatarajia. Ameamuwa kuwazawadia hii track. Iliyopikwa na @shirkomedia ndani ya jumba la maajabu @viberecordstz utaipata kwenye mitandao tofauti”

Comments

comments

You may also like ...