Header

Kwa mara ya kwanza Zari aizungumzia Video ya Diamond na Wema.

Mwanadada maarufu nchini ambaye ni Mjasiriamali Zarina Hassan a.k.a ZaritheBosslady kwa mara ya kwanza amezungumzia video fupi ambayo ilisambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Mzazi mwenzie Diamond Platnumz amaye alikua ni mpenzi wake akimkumbatia Wema Sepetu ambaye aliwai kuwa na Mahusiano nae ya kimapenzi hapo awali.

Akizungumza na kituo kikubwa cha habari nchini Uingereza, BBC Swahili mama huyo mwenye watoto watano amesema hakuwahi kumuuliza kitu chochote Diamond kuhusu ile Video kwasababu aliona ni kama kupoteza muda kwani kila kitu kilikuwa wazi.

“Hakuzungumza na mimi kitu chochote kuhusu ile video na mimi sikumuuliza kitu kwasababu niliona kama its very pointless so sikumuuliza kitu chochote” Alisema Zari.

February 14 Zarithebosslady kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza rasmi kuachana na Baba watoto wake Diamond Platnumz kwa kile alichodai kuwa ni kutokana na mfululizo wa matukio ya usaliti na kutokuheshimiwa na Diamond pamoja na Watoto wake.

Comments

comments

You may also like ...