Header

Sugu kutumikia kifungo jela kwa miezi mitano

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewahukumu Msanii wa muziki wa rap ambaye pia mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Osmund Mbilinyi a.k.a Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kwenda jela kifungo cha miezi mitano.

Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite ambapo Sugu na Masonga wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli katika mkutano wa hadhara.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo dhidi bya Rais kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika terehe 30 mwezi Disemba mwaka jana(2017) eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Comments

comments

You may also like ...