Header

Maamuzi ya Nyota wa Atletico Madrid yawashangaza wapenzi wengi wa Soka

Siku ya Jana Klabu ya Soka ya Atletico Madrid ilitangaza kufikia makubaliano na Klabu ya Dalian Yifang inayoshiriki Ligi kuu nchini China juu ya uhamisho wa Wachezaji Yannick Carrasco and Nico Gaitan kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

Gaitan, 30 alijiunga na Atletico Madrid Mwaka 2016 akitokea katika Klabu ya Benfica ya nchini Ureno huku Yannick Carrasco alijiunga na Atletico Mwaka 2015 akitokea Klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa.

Wapenzi wengi wa Soka wameshangazwa sana na usajili wa Carrasco kuelekea nchini China. Watu wengi huwa na imani kuwa Wachezaji wengi huenda nchini China kwa ajili ya kufata Pesa tu wala si kutaka kupata nafasi ya kucheza. Carrasco, 24 alikuwa ni Moja kati ya Wachezaji ambao walikuwa wanatazamwa kuja kuwa bora sana Duniani kulingana na kiwango alichoonesha akiwa Atletico Madrid.

Mwaka 2016 katika Michuano ya UEFA Champions League Carrasco aliisaidia Atletico kutinga hatua ya Fainali ya Michuano hiyo. Katika Mchezo wa Fainali dhidi ya Wapinzani wao Real Madrid Carrasco alitokea katika benchi na kufunga goli la kusawazisha dakika ya 79 lililoisaidia Atletico kufika hadi hatua ya Penati ambazo pia Carrasco alikuwa ndiye Mchezaji wa kwanza kupiga penati na kufunga kwenye hatua hiyo licha ya Atletico kukubali kufungwa na Real Madrid.

akiwa na Umri wa Miaka 24 tu Carrasco amefunga jumla ya Magoli 17 katika Michezo 81 huku akifunga Magoli 5 katika Michezo 22 aliyocheza katika Timu ya Taifa ya Ubelgiji ambayo ina wachezaji wengi wazuri wenye kugombania namba akiwemo Lukaku, Hazard kevin De Bruyne na nyota wengine.

Katika Mawazo mengi ya Mashabiki wanaona huenda ikawa ni Pesa au kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Atletico Madrid hivyo anajaribu kwenda katika Timu itakayomuhakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza ili aweze kupata nafasi katika Timu ya Taifa kwenye Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Comments

comments

You may also like ...