Header

“Napenda Mashabiki wangu waniite Linah sio Mama Tracey”;-Linah

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linah Sanga a.k.a Ndege Mnana amesisitiza kuwa licha ya kuwa na Mtoto anayeitwa Trace bado anapendelea kuitwa Linah badala ya Mama Tracey na Mashabiki wake hususani kwenye kazi

Akipiga story na Dizzim Online Staa huyo wa ngoma ya ‘Same Boy’ aliyoshirikiana na msanii mwenzie Recho amesema kuwa jina la Linah linamaana kubwa sana kwenye muziki wake hivyo aitwe jina hilo anapokuwa kazini na sio jina la Mama Tracey.

“Mimi napenda niitwe Linah kwenye maojiano au hata nikiwa nafanya show na sio jina la mwanangu Tracey kwasababu jina langu ndio linanipa ugali so sina buti kuendelea kulitumia hilo.

Aidha Linah ameongezea na kusema ujio wa Mtoto wake huyo umebadili sana Maisha yake kwa kiasi kikubwa sana.

Comments

comments

You may also like ...