Header

Banana Zorro aonekana kwenye dalili za ujio mpya

 

Staa na mkongwe wa muziki kutoka nchini Tanzania, Banana Zahir Ally Zorro ‘Zahir Ally Zorro’ ameanza kuonekana katika uwezekano wa kolabo ya wimbo kati yake na rapa na mwimbaji wenye majina tajwa na uwezo kubwa katika muziki ndani na nje ya Tanzania.

Baada ya kimya cha muda katika muziki wa mashabiki kutomsikia katika kazi zake binafsi, kupitia ukurasa wake wa Instagram jana aliweka ujumbe wenye ishara ya kuwa ipo kazi ambayo kashiriki itakayokwenda kwa jina ‘Asante’.

Kazi hiyo imehisiwa kuwashirikisha mwimbaji Nuruely na rapa Kala Jeremiah ambapo pia imeonekana kama kazi hiyo itakuwa ni chini ya Utayarishaji wa Prodyuza Zest kutoka Studio za Moja Moja Records.

Banana alipost picha na kuandika, “#asante @officialnuruelytz @kalajeramiah @shameh @gracevipodozi #mizikiyamiziki #mojamojarecords #zest”.

Comments

comments

You may also like ...