Header

Beka Flavour avutwa shati na ‘Kibenteni’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayefanya vizuri na ngoma yake ‘Kibenteni’, Bakari Katuti a.k.a Beka Flavour ametuliza shahuku yake ya kuachia wimbo mwingine kutokana na upya na kuendelea kufanya vizuri kwa wimbo wake huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Beka ameandika kuwa anayohamu ya kuachia wimbo mwingine na kisha akabainisha kuwa kuna kizuizi cha mashabiki kuendelea kupata raha kwa wimbo wake mpya wa Kibenteni kwa sasa.

Beka aliandika “Na hamuuuuuu sema Ngoja nitulie kwanza haraka haraka haina baraka #KIBENTENI link kwa bio yangu @faizaomaryofficial @travellah #levesmambo ni 🔥🔥🔥 @jonsambila @sirajizo”

Hata hivyo inaonesha wazi kuwa Beka ni hamu yake kuachia nyimbo kutokana na mfululizo mzuri wake wa kufanya hivyo kwakuwa tangu amesikika katika utendaji kazi kama msanii wa kujitegema(Solo Artist) tayari ameshaachia nyimbo zisizopungua tano ndani ya miezi tisa huku asilimia kubwa ya nyimbo hizo zikitoka sambamba na video.

Comments

comments

You may also like ...