Header

Chin Bees kuzindua album yake Ijumaa hii, kutoa nakala za bure kwa mashabiki

Rapper Chin Bees anatarajia kuzindua album yake mpya Ijumaa hii, March 2. Uzinduzi huo utafanyika Club Next Door jijini Dar es Salaam.

Chin Bees ambaye pia anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa uandishi wa nyimbo, yupo chini ya kampuni ya Wanene Entertainment ambayo imekuwa ikimsimamia kwa muda sasa. Album hiyo inatoka chini ya usimamizi wa kampuni hiyo.

Kwenye uzinduzi huo ambao utahudhuriwa na mastaa kibao, Bees pia atagawa bure nakala za album hiyo kwa mashabiki watakaohudhuria pamoja na kuionesha kwa mara ya kwanza video ya wimbo wake mpya.

Katika kipindi cha miaka miwili, Chin Bees anayetokea Arusha, ameibuka kuwa mmoja wa waimbaji waliochupikia kwa kasi huku nyimbo zake Pepeta, Kababaye, Nyonga na zingine zikimweka juu.

Comments

comments

You may also like ...