Header

Espanyol waendelea kuzamisha Jahazi la Real Madrid La Liga

Klabu ya Real Madrid imeendea kuongeza ‘Gap’ la alama dhidi ya Mahasimu wao Klabu ya Soka Barcelona baada ya hapo jana kukubali kichapo cha Goli 1-0 dhidi ya Espanyol kwenye Mchezo wa Ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga.

Real Madrid ambao walikuwa wameshinda Michezo Mitano mfululizo kabla ya kupoteza dhidi ya Espanyol  hapo jana walimpumzisha Nyota wao Cristiano Ronaldo ambaye hakucheza kabisa huku Zinadine Zidane akiwapa nafasi Vijana wengine kama Asensio, Hakimi pamoja na Lucas Vazquez.

Goli la Espanyol lilifungwa na Gerard Moreno katika Muda wa nyongeza wa dakika za mwisho na kuwanyima Real Madrid alama tatu huku wakiifanya iendelee kusalia nafasi ya Tatu ikiwa na Alama 51 nyuma ya Vinara Klabu ya Barcelona yenye alama 65 pamoja na Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya Pili wakiwa na alama 58.

Nguvu kubwa ya Klabu hiyo huenda ikahamishiwa katika Michuano ya UEFA Champions League baada ya kufanya vizuri katika Mchezo wa kwanza wa hatua ya Mtoano dhidi ya PSG kwa kuifunga Magoli 3-1 huku wakisubiri Mchezo wa marudiano Februari 6.

Comments

comments

You may also like ...