Header

Fahamu Sheria Mpya za UEFA zitakazoanza kutumika Msimu Ujao 2019

UEFA imetangaza Mabadiliko ya Michuano ya UEFA Champions League pamoja na ile ya UEFA Europa League, mabadiliko ambayo yataanza kutumika rasmi kuanzia Msimu ujao 2018-2019.

Kuanzia Msimu ujao Timu nne kutoka Ligi ya England, Hispania, Italia pamoja na Ujerumani zitafuzu Moja moja kuingia katika Makundi ya UEFA bila kucheza Michezo ya ‘Play offs’ kama ilivyokuwa Misimu iliyopita huku Ligi ya Urusi pamoja na Ufaransa zikitoa Timu mbili yaani iliyoshika namba Moja pamoja na namba Mbili huku Ligi ya Ureno, Ukraine, Ubelgiji pamoja na Uturuki zitatoa Timu Moja ambazo zilishinda Ubingwa Msimu huo.

Timu hiz0 tajwa hapo juu zitafanya Idadi ya Jumla ya Timu 24 ambazo zitaungana na Bingwa wa UEFA pamoja na  Europa Msimu wa Mwaka 2017-2018 (Msimu huu) na kufanya Jumla ya Timu 26 zitakazoshiriki Michuano hiyo Moja kwa Moja.

Kwa Upande wa Europa kwa sasa Timu 17 zitafuzu Moja kwa Moja kushiriki Michuano hiyo, Timu hizo zitapatikana kutoka katika Ligi kulingana na Idadi na Viwango katika Mgawanyo wa UEFA.

Ligi ya Hispania, Uingereza, Italia pamoja na Ujerumani zitatoa timu mbili ambazo zimeshika nafasi ya Tano na Sita katika Ligi zao ambazo kwa ujuma wake zitafanya kuwa Timu 10. Ligi za Russia, Portugal, Ukraine, Belgium, Turkey, Czech Republic na Switzerland zitatoa Timu Moja kila nchi na kufikisha Timu saba ambazo zitaungana na Timu 10 za Mwanzo.

 

Comments

comments

You may also like ...