Header

Mabantu waanza kwa kumzungumzia mrembo ‘Sundi’

Wakali wawili wa kuimba kutoka Tanzania, Muuh Mabantu na Twaah Mabantu ‘MABANTU’ wameachia video ya wimbo wao mpya kwa jina ‘Sundi’ kazi iliyoandaliwa katika Studio za BANNY MUSIC na video kuongozwa na LUCAS SWAHILI.

Wakali hao ambao ni ndugu kifamilia, wamekutana katika wimbo huo mpya ambao kwa mwaka 2018 unaweza kuwatambulisha rasmi kama wasanii walioamua kuianza safari ndefu kwa kazi yenye ubora na mwanzo mzuri wa kuandaa mazingira ya kutazamwa kwa jicho la ziada katika muziki.

Hata hivyo wasanii hao walishajihusisha na masuala ya kimuziki wakiwa chini ya kivuli cha kituo cha Mkubwa na Wanawe ambapo baadae ya muda walionekana kufanya kazi wakiwa nje ya kituo hicho.

Comments

comments

You may also like ...