Header

Makala ya Maisha ya Paul Walker yaanza kuandaliwa

Paramount Network ya Marekani na mtengenezaji wa filamu maarufu Derik Murray wameshirikisha kuandaa makala katika mfumo wa filamu kwa jina “I Am Paul Walker,” itakayozungumzia maisha ya umaarufu na kifo cha ghafla cha Muigizaji  wa ‘Fast and the Furious’ Paul Walker.

Makala hiyo ya Filamu itajumuisha mahojiano kutoka kwa washiriki wenza wa filamu wa Paul na marafiki zake wa karibu ambapo Adrian Buitenhuis atakuwa muongozaji wa filamu hiyo na Jon Slusser pamoja na Jaimee Kosanke watasimama kama watayarishaji wakuu.

Maelezo zaidi na ya kina kuhusu kukamilia na ujio wa filamu hiyo, ikiwa ni pamoja na tarehe rasmi ya kuingia sokoni itatangazwa hivi karibuni.

Comments

comments

You may also like ...