Header

Roger Federer ampiku Ronaldo na kunyakua Tuzo ya Mwanamichezo bora

Mcheza Tenisi anaeshikilia nambari Moja Duniani kwa ubora upande wa Wanaume Roger Federer ameshinda Tuzo Mbili katika Tuzo za  Laureus World Sports Awards zilizofanyika Usiku wa Jana Mjini Monaco nchini Ufaransa.

Mswiswi huyo mwenye Miaka 36 ameshinda Tuzo mbili, Mwanamichezo bora wa Mwaka 2017 ‘Sportsman of the Year’ akiwapiku:- Mchezaji wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo, Mwanariadha kutoka Uingereza Mo Farah, Mwendesha Baiskeli Chris Froome kutoka England pamoja na Dereva wa Mbio za Magari za Formula 1 Lewis Hamilton. Kipengere kingine alichoshinda Federer ni ‘Comeback of the Year’.

Kwa Upande wa Wanawake Mwanadada Serena Williams ameshinda Tuzo ya Mwanamichezo bora kwa upande wa Wanawake na kufanya Tuzo hizo kutawalaiwa na Wachezaji wa Tenisi.

Federer ambaye ni Mshindi mara 20 wa Gland Slam amefanya vizuri sana Mwaka 2017 baada ya kuwa na Mfululizo wa Misimu 7 ambayo hakutwaa Taji lolote kubwa, Mwaka Jana alishinda Ubingwa wa wazi wa Michuano ya Australia ‘Australian Open 2017’ pamoja na Ubingwa wa Wimbledon.

Comments

comments

You may also like ...