Header

Sugu aenda Jela na kuacha maneno ya Jay-Z uraiani

Rapa na mkongwe wa muziki wa Rap na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Osmund Mbilinyi a.k.a Sugu  ameacha ujumbe kutoka kwa rapa na mjasiriamali kutoka Marekani, Jay Z kabla ya kwenda jela kutumikia kifungo cha miezi mitano kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John P. Magufuli kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwaka Jana.

Hukumu ya Sugu ilimhusu pia Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kwa kosa hilo lilifanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika terehe 30 mwezi Disemba mwaka jana(2017) eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Katika kupitia ukurasa wake imeonekana kuwa post yake ya mwisho kwenye mtandao wa Instagram, Sugu aliweka picha yenye ujumbe kutoka kwa Jay-Z uliosema “THE GENIUS THING THAT WE DID WAS, WE DIDN’T GIVE UP -JAY-Z”

Hata hivyo Sugu inawezekana kabisa asipate nafasi ya kutumia mitandao ya kijamii au kuweka chochote katika akaunti yake hiyo kwa muda usiopungua miezi mtano mpaka pale atakapomaliza kutumikia adhabu hiyo.

Comments

comments

You may also like ...