Header

Enock Bella kwa Mkubwa Fella, heshima iliazia katika tarehe zao za kuzaliwa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyekuwa miongoni mwa wanakikundi cha Bendi ya Yamoto, Enock Bella na Meneja wa kituo cha kulea na kuibua vipaji cha Mkubwa na Wanawe ‘Mkubwa Fella’ wamenaungana katika siku moja na ya pekee katika maisha yao.

Tofauti ni umri na nafasi walizonazo katika tasnia ya muziki Tanzania lakini wawili hao moja ya kitu kinachowafanya wawe na furaha ya pamoja ni kufanana kwa tarehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwao ambayo ni tarehe 1 Mwezi Machi tofauti ikiwa ni mwaka, miaka kadhaa iliyopita.

Hata hivyo mahusiano yao mazuri yanaweza kuwatambulisha kama baba na mwana kwani siku zote heshima imeonekana kutawala kati yao na wanategemewa kushirikiana katika hali ya kutegemeana katika tasnia ya muziki Tanzania kwakuwa walishafanya hivyo kabla na wanaonekana kuwa katika uwezekano mkubwa wa wao kufanya hivyo pale msaada unapohitajika kwa pande zote mbili.

Comments

comments

You may also like ...