Header

Justin Bieber asiye huru nchini China anasherekea siku sawa na Lupita Nyong’o

Staa wa muziki wa Pop kutoka Canada, Justin Drew Bieber ‘Justin Bieber’ leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambapo anatimiza umri wa miaka 23 na msanii huyo mbali na umaarufu Duniani alionao kupitia muziki wake, hana mahusiano mazuri na nchi ya China.

Taarifa rasmi iliyokuwa ikijibu swali la mtu mmoja aliyeulizwa swali kuhusu Justin kutoa Buruani nchini kuelekea Wizara ya Utamaduni nchini humo, alijibiwa kuwa Justin amepigwa marufuku kutumbuiza nchini China kutokana na mlolongo wa matukio yake ya utovu wa nidhamu ambapo wizara hiyo haimpi nafasi msanii mwenye rekodi ya matukio mengi ya kinidhamu kutumbuiza nchini humo.

Hata hivyo Justin Bieber katika siku ya leo ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake anaungana na muigizaji maarufu mwenye asili ya nchini Kenya, Lupita Nyong’o kwakuwa siku ya leo anatimiza umri wa miaka 34.

Comments

comments

You may also like ...