Header

Nay wa Mitego na Diamond Platnumz waongoza idadi ya nyimbo zilizofungiwa Tanzania

Baraza la Sanaa Tanzania BASATA imetoa Orodha ya nyimbo zilizo nje ya maadili ya Kitanzania za wasanii ambazo zimendaliwa na wasanii hao kwenda kwa vyombo mbali mbali vya Matangazo na mitandao ya kijamii.

Sababu zimebainisha kuwa Nyimbo hizo zimebeba maudhui yenye tafsiri kinyume na maadili na kanuni za huduma za utangazaji(maudhui)2005 nchini Tanzania na kwa yeyote katika chombo husika atakayecheza nyimbo hizo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa chini ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA).

 

Msanii Diamond Platnumz na Nay wa mitego ni wasanii walioingiza nyimbo zaidi zaidi ya wasanii wengine kwakuwa Nay ngoma zake zilizofungiwa ni Pale Kati Patam,  Makuzi na Mikono Juu ambapo kwa Diamond ngoma zilizofungiwa ni Waka waka na Hallelujah.

Orodha ya Nyimbo hizo ni:

“`1.Hallelujah – Diamond Platnumz

 1. Waka waka – Diamond Platnumz
 2. Kibamia – Roma Mkatoliki
 3. Pale Kati Patam – Nay wa Mitego
 4. Hainaga Ushemeji – Manfongo
 5. I am Sorry JK – Nikki Mbishi

“`7.Chura – Snura

 1. Tema mate tumchape – Madee
 2. Uzuri wako – Jux
 3. Nampa papa – Gigy Money
 4. Nampaga – Barnaba
 5. Makuzi – Nay wa Mitego
 6. Nimevurugwa – Snura
 7. Bongo Bahati Mbaya – Young Dee
 8. Mikono Juu – Nay wa Mitego

Orodha hii ya ngoma zilizofungiwa kuchezwa katika vyombo vya habari nchini Tanzania imekusanya idadi ya ngoma 15 zilizotoka ndani ya miaka 5 mpaka sasa.

Comments

comments

You may also like ...