Header

Wizkid kushiriki kwa mara ya kwanza tamasha la Coachella mjini California

Mapema mwaka huu, Coachella alitoa orodha ya mastaa wa muziki watakao shiriki katika tamasha lao hilo la kila mwaka. Orodha hiyo ilimjumuisha Staa wa muziki wa afropop StarBoy kutoka Nigeria Wizkid.

StarBoy ambaye kwa mwaka huu atatimiza umri wa miaka 28 na wakali wengine kutoka Marekani ambao ni pamoja na The Weeknd, anatarajiwa kuwakilisha vilivyo muziki wa Afrika katika tamasha hilo litakalofanyika siku ya Jumamosi, Aprili 14 na 21 katika ukumbi wa Dola Polo Club huko Indio, California, Marekani.

Coachella(Coachella Valley Music and Arts Festival) ni tamasha kubwa zaidi linaloangazia la muziki na Sanaa kwa ujumla, lenye umaarufu mkubwa, na lenye manufaa zaidi katika burudani ya muziki nchini Marekani na duniani kote.

Mwaka jana(2017) tamasha hilo lilihudhuriwa na watu wasiopungua 250,000 na lilitajwa kuingiza kiasi cha pesa  cha $ 114.6 milioni.

Comments

comments

You may also like ...