Header

“Hanscana Angekuwa msanii, ningempa offer ya Video kali” – Director Nicklass

Mwongozaji wa video za muziki kutoka Tanzania, Nicko MMbaga ‘Director Nicklass’ ametoa sababu za alichokiandika kwenda kwa muongozaji mwenzake wa video za Hans Richard ‘Director Hanscana’.

Akipiga Stori na Dizzim Online, Nicklass amesema kuwa alichokiandika mtandaoni juu ya kumpa Pongezi Hanscana kimetoka moyoni na haoni sababu ya muongozaji mwenzake kufanya vizuri hasimpe hongera zake.

“kusema ukweli Hascana amefanya kazi kubwa sana kwa upande wa video za muziki, kwa juu juu mtu unaweza kudhani Director kufanya video zisizopungua mia ni kitu kidogo na cha kawaida lakini sisi tunaojua ugumu wa kazi hii lazima tutoe pongezi kwa aliyefikia hatua hiyo. Hascana kafikisha idadi kubwa sana ya video na nikaona sio mbaya kama nitampa pongezi zake, Angekuwa msanii ningempa offer ya Video kali” Amesema Director Nicklass.

Wiki iliyopita Hascana aliweka picha yenye ujumbe wa kuwa amefikisha jumla ya video za muziki 100 zilizofanya vizuri kuanzia mwaka 2014 mpaka sasa kitu ambacho Nicklass amekipokea kwa ukubwa na kutoa pongezi kwa Hascana.

Comments

comments

You may also like ...