Header

Harmonize aomba radhi juu ya kolabo yake na Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania(Bongo Fleva) na Staa wa ngoma ya ‘Aiyola’ Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ ameomba radhi juu ya kutoachia wimbo wake kwa jina ‘Kwangwaru’ uliomshirikisha Diamond Platnumz.

Wimbo huo kwa mujibu wa Harmonize ulitarajiwa kutoka tarehe 1 March mwaka huu kitu ambacho kilisubiriwa na wengi ambapo katikati mwa siku tajwa ya kutoka kwa wimbo, Harmonize aliutumia ukurasa wake wa Instagram kuwaomba radhi mashabiki na wadau wote waliosubiria ujio huo kwa madai kuwa mambo hayajaenda kama yalivyopangwa.

“🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️ NIWAOMBE RADHI NDUGU ZANGU KUTOKANA NA SABABU ZILIZO KANDO YA UWEZO WETU NGOMA HII HAIJABAHATIKA KUTOKA LEO NAJUA TULIO WENGI TUNAINGOJEA SANA….!!! ILA NDIO INAKUWAGA HIVYO WAKATI MWINGINE MAMBO MAZURI HAYAHITAJI HALAKA….!!! NIKUOMBE UPENDEKEZE SIKU YAKO ILA ISIWE YA MBALI SANA….!!! MANA TUKISOGEZA MBALI ZAIDI UTAMU NAO UNAISHAGA….!!! #HARMONIZE & #SIMBA MUDA WOWOTE ⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚⌚🎵🎶” Aliandika Harmonize.

Hata hivyo Harmonize baada ya kuomba radhi na kuwataka mashabiki wataje siku ya kutoka kwa wimbo huo, baadhi waliweka maombi ya kuwa wimbo huo utoke tu sasa hivi dalili zilizoonesha kuwa mashabiki wanaingoja kwa hamu kolabo hiyo na hawana tena muda wa kusubiria.

Comments

comments

You may also like ...