Header

Jason Derulo alamba Shavu la Kombe la Dunia 2018

 

Staa wa muziki kutoka nchini Marekani, Jason Joel Desrouleaux ‘Jason Derulo’ amepewa hati ya kurekodi wimbo rasmi wa Kombe la Dunia ya 2018 ya FIFA.

Huu ni muendelezo wa Mastaa wakubwa Duniani kushiriki katika misimu ya Mashindano ya Kombe la Dunia ambapo Pitbull na Shakira walishapata shavu kama hilo ambalo Jason Derulo atahusika kuimba wimbo wa michezo kwa jina “Colours, ambao utaonyeshwa katika mashindano yajayo huko nchini Urusi.

Wimbo huo rasmi wa mashindano hayo ya 2018 unatarajiwa kutoka Machi 16, na Jason Derulo atatumbuiza kwa wimbo huo kwenye sherehe ya ufunguzi wa Kombe la Dunia huko mjini Moscow, Urusi. Jason Derulo ameongeza kuwa wimbo huo wa ‘Colours’ utakuwa kwenye album yake mpya.

Comments

comments

You may also like ...