Header

“Like Father Like Son!” Mtoto wa Cristiano Ronaldo atamani kuwa kama Baba yake

Cristiano Ronaldo Junior ambaye ni Mtoto wa Staa wa Soka kutoka Klabu ya Real Madrid pamoja na Timu ya Tifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameonyesha Dalili zote za kutaka kuwa kama Baba yake pindi akiwa Mkubwa.

Ronaldo kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa kijamii wa Twitter, Siku ya Jana aliweka Picha ya Mtoto wake ambaye alionekana akiwa sehemu ya Mazoezi huku akiwa amevua Shati na kutunisha Misuli kama alivyowai kufanya Baba yake katika Fainali ya Michuano ya UEFA 2016 wakati akishangilia goli alilofunga kwa Penati dakika za mwisho, Ronaldo aliambatanisha ujumbe huu katika Picha hiyo;

“Cristiano Jr amesema, Baba nitakuwa kama wewe, Vipi nyie mnaonaje??”. Alimaliza kwa kuwauliza Mashabiki zake ambao waliweka Majibu yao Tofauti.

Mtoto huyo mwenye Miaka 7 sasa amekuwa akionyesha kila Dalili kuwa atakuja kuvaa Viatu vya Baba yake hususani katika Soka, Cristiano Jr ameonekana mara nyingi akifanya Mazoezi na Baba yake Uwanjani na hata wakiwa Gym. Lakini pia video nyingi zimekuwa zikimuonesha akicheza na kufunga aina ya Magoli kama Ronaldo.

Comments

comments

You may also like ...