Header

Obby Obeddy ‘Obby’ ajipanga kuitumia nafasi ya Muziki wa Injili iliyoko Tanzania

Msanii wa muziki wa Injili kutoka Nchini Kenya na Staa wa ngoma ‘Nicheke’ Obed Bosire Omoro a.k.a Obby Obeddy  ‘Obby’ amejipanga kuachia kazi mpya na kuzungumzia mipango yake kimuziki kwa anachokiona katika muziki wa Injili nchini Tanzania.

Akipiga Stori na Dizzim Online, Obby amesema kuwa lengo lake linabaki katika kusambaza neno la Mungu kupitia muziki wake na kuongeza kuwa katika hatua zake za kufanya hivyo amegundua ipo nafasi kubwa ya wazi inayoweza kuruhusu muziki wake kuwafikia watanzanian wengi kwakuwa ameona nguvu kubwa ya wadau wa muziki inawekwa katika kuwasikiliza wasanii wanaofanya muziki wa kidunia kwa asilimia kubwa.

“Nimeona nafasi kubwa nchini Tanzania, Wasanii wa muziki wa kulitangaza neno kama ninavyo fanya mimi sio wengi huko kama vyenye iko hapa Kenya, then it’s in my plans kuwafikia wa-Tz kwa sasa huku as i set my strong journey for my gospel music kufika nchi nyingine za mbali” Amesema Obby.

Kwa sasa Obby anafanya vizuri na kazi yake mpya kwa jina ‘Penzi’ uliotayarishwa na Prodyuza YO Alex katika studio Drama House Music. Video ya wimbo huo imetayarishwa na kuongozwa na Director Omae Lion chini ya kampuni ya Maefamm Music.

Comments

comments

You may also like ...