Header

Rick Ross alazwa Hospitalini kwa tatizo la kushindwa kupumua

Rapa kutoka nchini Marekani, William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’ amelazwa hospitalini kwa matibabu akiwa ni mwenye hali mbaya kiafya baada ya kuchukuliwa kwa dharura katika eneo la Miami nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Mtandao wa TMZ, mtu mmoja kutoka nyumbani kwa rapa huyo alipiga simu ya dharura( 911) mida ya usiku(3:30AM) majira ya Marekani siku ya Alhamisi na kutoa taarifa kuwa Ross amezidiwa na tatizo la kushindwa kupumia kwani alikuwa kipumua kwa shida sana kiasi ambacho hakuwa na uwezo wa kuongea.

Ripoti ya mtandao huo iliongeza kuwa, Rick alipelekwa hospitali kwa kwa msaada wa gari la wagonjwa na alipokea matibabu ya awali ya kusaidiwa ili aweze kupumua  na akagundulika kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Mapafu ‘Pneumonia’.

Katika kufatilia ukweli wa taarifa za Rapa Rick Ross kulazwa, mtu mmoja kutoka katika familia ya Rick Ross alikanusha taarifa za kuwa Rick Ross amelazwa hospitalini.

Comments

comments

You may also like ...