Header

Tale akamilisha Mixing na Mastering ya wimbo ‘Check It’ wa Chin Bees

Staa wa muziki wa Rap na Trap kutoka Tanzania anayefanya kazi chini ya lebo ya Wanene Entertainment, Chin Bees ameachia video ya wimbo wake kwa jina ‘Check it’ uliotayarishwa na Prodyuza Goncher kwa kushirikiana na Darsh aliyehusika katika mpangilio wa audio ya wimbo.

Katika kukamilisha audio ya wimbo huo Mixing na Mastering amehusika Engineer Sarthak Tale ambapo video ya wimbo imeongozwa na Director Destro chini ya Wanene Films.

Hata hivyo katika video Chin Bees ameonekana kupendeza sana kwa mavazi ambapo Costume Design imekamilishwa na Mwanamitindo Rio Paul.

Itazame video ya wimbo huo mpya.

Comments

comments

You may also like ...