Header

Uongozi wa WCB Wasafi wazungumzia kufungiwa kwa nyimbo mbili za Diamond Platnumz

Uongozi wa unaosimamia shughuli za muziki wa Staa wa Bongo Fleva ‘Diamond Platnumz’ umezungumzia taarifa za kufungiwa kwa nyimbo mbili za Diamond Platnumz katika orodha ya nyimbo 15 zilizoorodheshwa kuwa hazitaruhusiwa kuendelea kuchezwa katika vyombo vya habari nchini Tanzania kwa sababu za kimaadili.

Taarifa za kuFungiwa kwa nyimbo hizo zikiwemo nyimbo mbili za Diamond Platnumz ambazo ni Hallelujah iliyomshirikisha Morgan Heltedge na Waka Waka iliyomshirikisha Rick Ross ni kwa mujibu wa Barua kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania(TCRA) kuelekea Radio moja mjini Dodoma iliyomesema nyimbo hizo zimefungiwa kwa ushauri kutoka kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo kupitia ukurasA wa Instagram, Meneja wa Msanii huyo, Sallam SK ameweka ujumbe kuwa wao kama wahusika hawajapokea barua ya taarifa ya kuwa nyimbo hizo zimefungiwa na zimefungiwa kwa sababu zipi.

“Habari za muda huu waungwana. Tumepigiwa simu na vyombo vya habari kila sehemu kuulizwa juu ya nyimbo mbili za Diamond kufungiwa, nimeona tukiwa kama taasisi huwaga tunafanya vitu kwa kutokukurupuka sie kama @wcb_wasafitulipoona taasisi yetu inakuwa kubwa tukaomba ulezi kwa @paulmakonda ambae ni kiongozi wa serikali mwenye kupenda maendeleo ya vijana, kwahiyo nyimbo zote za WCB kabla ya kutoka lazima mlezi wetu azipitie, kuna nyimbo nyingi ameshazizuia na zinazotoka basi ameridhia yeye binafsi zitoke, kwahiyo sioni sababu ya nyimbo ya Hallelujah na Waka kufungiwa kama inavyosemekana maana sisi hatujapata barua ya kuwa nyimbo hizo zimefungiwa na kwa sababu ipi. Kama kweli zimefungiwa basi mlezi wetu ataweza kuongea mengi zaidi yangu mimi. Nawatakia Weekend njema. Pichani nipo na @babutale tumevaa jezi za Lipuli by @speshoz” Ameandika Sallam Sk.

Habari za muda huu waungwana. Tumepigiwa simu na vyombo vya habari kila sehemu kuulizwa juu ya nyimbo mbili za Diamond kufungiwa, nimeona tukiwa kama taasisi huwaga tunafanya vitu kwa kutokukurupuka sie kama @wcb_wasafi tulipoona taasisi yetu inakuwa kubwa tukaomba ulezi kwa @paulmakonda ambae ni kiongozi wa serikali mwenye kupenda maendeleo ya vijana, kwahiyo nyimbo zote za WCB kabla ya kutoka lazima mlezi wetu azipitie, kuna nyimbo nyingi ameshazizuia na zinazotoka basi ameridhia yeye binafsi zitoke, kwahiyo sioni sababu ya nyimbo ya Hallelujah na Waka kufungiwa kama inavyosemekana maana sisi hatujapata barua ya kuwa nyimbo hizo zimefungiwa na kwa sababu ipi. Kama kweli zimefungiwa basi mlezi wetu ataweza kuongea mengi zaidi yangu mimi. Nawatakia Weekend njema. Pichani nipo na @babutale tumevaa jezi za Lipuli by @speshoz

A post shared by "Mendez" ♠️ (@sallam_sk) on

Hata hivyo SK ameeleza kuwa kutokana na ukubwa wa WCB Wasafi kama taasisi, wamekuwa wakimshirikisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika kuzingatia maadili ya nyimbo kutoka kwa wasanii wao hivyo kila nyimbo zilizotoka zimeridhiwa na mkuu wa mkoa huyo ambaye ushirikiana nao kama mlezi wa taasisi hiyo pale anapohitajika kutoa usaidizi ulio katika maadili na kuzingatia sheria za nchi.

 

 

Comments

comments

You may also like ...