Header

King Kaka arudi tena Tanzania, aungana na Barnaba Classic

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, Kennedy Ombima ‘King Kaka’ amedondosha video ya wimbo wake mpya uliomshirikisha Staa wa ngoma ya ‘Lover Boy’, Barnaba Boy Classic kwa jina ‘Radhi’.

Video ya wimbo huo imeongozwa na kumakilishwa na Director kutoka Tanzania na mmiliki wa kampuni ya  Video ya Joh Films, ‘Joowzey’ ambapo Barnaba amehusika katika utayarishaji wa audio chini ya Studio zake za High Table Sound na umaliziaji kufanyika chini ya BBSound.

Kolabo hii yake na Barnaba inamfanya King Kaka kuwa msanii kutoka Kenya kuwa na kolabo nyingi na wasanii wa Tanzania kwakuwa Alishashirikiana na Jay Moe, G Nako, Joh Makini,Rich Mavoko na Barakah The Prince.

Itazame video ya wimbo huo mpya

 

Comments

comments

You may also like ...