Header

‘Tangu zamani wasanii walikuwa wanaweka rangi kichwani’ Bushoke-;

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Ruta Maximilian Bushoke  a.k.a Bushoke, amezungumzia suala la mastaa kubadili mionekano yao ya Nywele.

Akipiga Story na Dizzim Online msanii huyo amesema kwake anaona ni kitu cha kawaida tu kwasababu haijaanza sasa, tangu zamani wasanii walikuwa wanaweka Rangi tofauti tofauti kwenye nywele zao.

“Nimeona Mastaa wengi wakibadili rangi za nywele zao ila mimi naona sawa wao kufanya vitu tofauti hasa kwa wasanii wanaangaliwa ingawa sio mambo mageni, yameanza zamani kwa hiyo watu tu wameamua kurudia hiyo style.” Amesema Bushoke.

Bushoke kwasasa amejikita zaidi kwenye biashara zake ingawa bado pia yupo kwenye Muziki.

Comments

comments

You may also like ...