Header

AliKiba atumika kama mfano kati ya wasanii wanaozingatia Maadili

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ ametumika kama mfano wa kuwa amekuwa akifanya shughuli zake za muziki na sanaa kwa ujumla bila kukiuka sheria za kimaadili tofauti na wasanii wengine baadhi walio kumbana na adhabu ya kazi zao baadhi kufungiwa kwa sababu za kukiuka maadili ya kitanzania.

Akizungumza kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amesema kuwa msanii kufika kimataifa inawezekana bila kutumia kazi zilizoandaliwa katika sura ya kwenda kinyume na sheria ya kimaadili ya Tanzania na kumtolea mfano AliKiba.

“Kwa mfano Alikiba ni msanii mkubwa wa kimataifa, anaiwakilisha nchi vyema, lakini haimbi nyimbo lugha chafu wala video ambazo hazina maadili. Sisi kama wizara tunataka sanaa iende pamoja na ukuaji wa maadili ya nchi – tutoe burudani lakini tulinde utamaduni wetu.” – Naibu Waziri Juliana Shonza” Amesema Mhe. Juliana Shonza.

Comments

comments

You may also like ...