Header

TID athibitisha ujio wa kolabo yake na Staa kutoka Nigeria

Mkongwe Wa Muziki kutoka nchini Tanzania, Khalid Mohamed ‘TID’ ametoa taarifa kuwa yuko nchini Ujarumani na ni katika hatua za mwisho za kolabo yake na Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, anayefanya shughuli za muziki wake nchini humo ‘Slimm Pizzle’.

Kolabo hiyo ya wimbo inayokwenda kwa jina ‘Live My Life’ imetayarishwa na Producer Smart Khiddy ambapo TID ameweka picha katika ukurasa wake wa Instagram na kudai kuwa wameshootvideo na mshabiki wakae tayari.

TID akiwa Studio na Slimm Pizzle

“On set with the Crew after Video shoot #livemylife featuring @slimmpizzleofficial somewhere in Europe stay tune for Positive Staff …Mjipange” Aliandika TID.

TID amekuwa nchini Ujerumani kwa mida usiopungua wiki sasa na hatimaye ameamua kutamatisha kwa maneno hayo kuwa kinachokuja kutoka kwao kitakuwa sio kidogo kwakuwa ni kolabo ya wasanii wenye uwezo na wenye kuwakilisha mataifa yao yenye sifa kubwa za kimuziki katika Bara la Afrika na Duniani kwa sasa.

Comments

comments

You may also like ...